Home / Announcements / Tangazo Muhimu kwa Wanafunzi Wote (Wapya na Wanaoendelea)

Tangazo Muhimu kwa Wanafunzi Wote (Wapya na Wanaoendelea)

Chuo Kinapenda Kuwatangazia Wanafunzi Wote Kwamba Mitihani ya Supplementary (Supplementary Exams) na Mitihani Maalum (Special Exams) Itaanza Kufanyika Kuanzia Siku ya Jumatatu ya Tarehe 10/09/2018. Wanafunzi Wote Wenye Supplementary na Special Exams wanatakiwa kuwepo kuanzia siku hiyo. 

Kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo kwa Mwaka wa Kwanza (First Year), Wanatakiwa Kuanza Kuripoti Kuanzia Siku ya Jumatatu ya Tarehe 08/10/2018. Joining Instructions Zinapatikana Kwenye Website hii ya Chuo. Majina Ya Wanafunzi waliochaguliwa Kwa Mara ya Pili yamewekwa kwenye Mtandao. Mnahimizwa Kusoma Masharti Yote Yaliyomo kwenye Joining Instruction ili kufuata utaratibu na Masharti ya Chuo kuepuka usumbufu.

Kwa Wanafunzi wanaoendelea (Continuing Students), Chuo Kitafunguliwa Siku ya Jumatatu Tarehe 15/10/2018. 

Mnakumbushwa, Sheria Zote Zitaendelea Kufuatiliwa Kwa Karibu Zaidi Hususan kwenye Mavazi, Vitambulisho na Mengine ya Msingi.

 

Imetolewa na 

KURUGENZI YA MAFUNZO