Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

BODI YA USHAURI YA FETA YAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA FETA.

Imewekwa: 21 October, 2026
BODI YA USHAURI YA FETA YAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA FETA.

Bodi ya ushauri ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA ) chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Blandina Lugendo  imeketi 15 Oktoba,2026 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Wakala.

Pamoja na mambo mengine Bodi imepitia na kushauri taarifa ya Mtendaji Mkuu wa FETA iliyokuwa na sehemu tatu Taarifa ya mendeleo ya taaluma, Taarifa ya masuala ya kiutawala pamoja na Taarifa ya fedha.

Baada ya kikao hiko Wajumbe wa bodi walipata fursa ya kutembelea sehemu ya uzalishaji wa vifaranga vya samaki, ukuzaji wa samaki wazazi na mabwawa ya kufugia samaki aina ya sato na kambale.