Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Kampasi ya Gabimori

Kuhusu FETA Gabimori

Kituo hiki cha Gabimori kilianza kujengwa toka mwaka wa fedha 2011/2012 na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kupitia Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding – MoU) baina ya Wizara na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara kwa kusudi la kutoa mafunzo kwa wagani, wafugaji na wavuvi.

Katika Makubaliano hayo ilibainishwa kuwa punde ujenzi wa kituo utakapofikia hatua ya kuanza kutumika, Wizara itakabidhi uendeshaji kwa Wakala za Mafunzo chini ya Wizara. Kutoka kipindi kilipoanza kujengwa mpaka Aprili 2014, kituo kilikuwa chini ya usimamizi wa Idara ya Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya. Baadaye Juni 2014, kituo kilikabidhiwa rasmi kwa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) ili kiweze kutoa elimu na mafunzo ya Uvuvi.

Utoaji wa mafunzo ya muda mfupi ulibarikiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luaga J. Mpina (Mb) mnamo tarehe 11/12/2019. Baada ya hapo, mafunzo ya muda mfupi ya ufugaji samaki yaliendelea kufanyika. Mafunzo hayo yalianza tarehe 10/12/2019 mpaka 19/12/2019. Mafunzo hayo yalijumuisha washiriki ishirini na tano (25).

Kozi zinazopatikana katika Kampasi yetu ya Gabimori

Kozi Ndefu.

Mpaka sasa, Taasisi haijaanza kutoa mafunzo ya muda mrefu kutokana na kutokidhi vigezo vya (NACTVET).

Kozi Fupi.

  • Ufugaji wa Samaki

Mahali Kampasi Inapopatikana

Kampasi ya Gabimori inapatikana katika kijiji cha Kyangasaga , Wilaya ya Rorya.katika mkoa wa Mara

  • Mratibu wa Kozi :        Hashimu Tengeni, 0742759677, hashimu.tengeni@feta.ac.tz
  • Meneja wa Kampasi:  Hashimu Tengeni, 0742759677, hashimu.tengeni@feta.ac.tz
  • S. L. P 22, Shirati,Rorya,Mara.
  • Barua Pepe: gabimori@feta.ac.tz