Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Kampasi ya Kigoma

Kuhusu FETA Kigoma

Kampasi ya FETA Kigoma, pia inajulikana kama Kampasi ya FETA Kibirizi, ilianzishwa na Serikali mwaka 2013 kufuatia kuanzishwa kwa wakala. Kampasi ya Kibirizi ilibadilishwa kutoka karakana ya awali ya ujenzi wa boti ya Kibirizi kuwa taasisi ya mafunzo.

Kampasi hiyo imekuwa kituo cha umahiri  katika elimu na mafunzo ya uvuvi na ufugaji wa viumbe kwenye maji katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. FETA Kigoma inatoa mafunzo ya muda mrefu katika teknolojia ya ufugaji wa viumbe vya majini pamoja na programu fupi kama vile waendeshaji wa vyombo vidogo vya majini, ambazo zimeidhinishwa na TASAC.

Mnamo mwaka 2014, FETA Kibirizi ilisajiliwa na kupata ithibati ya NACTVET kwa namba ya usajili REG/SAT/003 ili kutoa mafunzo mbalimbali katika teknolojia za uvuvi na ufugaji wa viumbe kwenye maji katika ngazi za Astashahada na Stashahada (Ngazi Ya NTA IV, V na VI).

Kozi zinazopatikana katika Kampasi yetu ya Kigoma

Kozi Ndefu

  1. Aquaculture Technology

Kozi Fupi

  1. Fish Farming
  2. Small Vessel Operators

Mahali Kampasi Inapopatikana

Kampasi ya Kibirizi ipo karibu na Mwalo wa Samaki wa Kibirizi, katika Mtaa wa Kibirizi ndani ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kandokando ya ufukwe wa Ziwa Tanganyika.

  • Mratibu wa Mafunzo:   Mr.Emmanuel Josia,0710634111, emmanuel.hamis@feta.ac.tz
  • Mawasiliano ya Ofisi ya Udahili:  0763208746  admission.kibirizi@feta.ac.tz
  • Mawasiliano ya Ofisi ya Mitihani:  0756208426 , rudia.shimba@feta.ac.tz
  • Campus Manager: Mr. August Shirima, 0758390788, august.shirima@feta.ac.tz
  • S.L.P 545, Kigoma,
  • Barua Pepe: kibirizi@feta.ac.tz