Kwa niaba ya FETA, ninayo furaha kubwa kukukaribisha kwenye tovuti yetu rasmi. Taasisi yetu imejipambanua kuwa kitovu cha umahiri katika elimu na mafunzo ya uvuvi na ufugaji viumbe maji katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa kuendeleza uvuvi endelevu, ufugaji viumbe maji, na utafiti wa rasilimali za maji, sambamba na kuhamasisha ubunifu na ushirikishwaji wa maarifa katika sekta hii.
Tumejizatiti katika kuunga mkono jamii yetu ya wanafunzi, watafiti, wadau na washirika kwa kutoa rasilimali za kuaminika, kufanya tafiti-tumizi, na kujenga fursa za ushirikiano. Kupitia programu na miradi yetu, tunalenga kuchangia katika maendeleo endelevu ya sekta ya uvuvi na mifumo ya ikolojia ya maji, ili kuhakikisha usalama wa chakula na riziki kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Tunakuomba utumie muda wako kuvinjari kwenye tovuti yetu, kufahamu zaidi kuhusu kazi zetu, na kujiunga nasi katika dhamira yetu ya kutoa elimu na mafunzo katika ufugaji viumbe maji, teknolojia na usimamizi wa uvuvi, kufanya tafiti-tumizi na kutoa ushauri elekezi kwa lengo la kuendeleza uvuvi endelevu na sekta shirikishi. Ushiriki na msaada wako ni wa thamani kubwa katika jitihada zetu za kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii.
Karibu sana, na asante kwa kuwa sehemu ya safari yetu.
Wasalaam,
Dkt. Semvua Isa Mzighani
Mtendaji Mkuu
Watembeleaji wa Mwezi
Idadi ya Wanafunzi
Program Zilizotolewa
Idadi ya Wafanyakazi