Kuhusu Kampasi ya FETA Mikindani
Mnamo mwaka 2008, karakana ya boti ya Mikindani ilichukuliwa na Kituo cha Maendeleo ya Uvuvi cha Mbegani ili kuwa kituo chake cha pembezoni. Mnamo mwaka 2012, karakana hiyo ya Mikindani iligeuzwa kuwa Kampasi ya FETA Mikindani na kujumuishwa chini ya FETA (Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi) ili kuwa moja ya kampasi za wakala, kufuatia kuanzishwa kwake.
Hadi sasa, Kampasi ya FETA Mikindani imekuwa chuo cha mafunzo kinachotoa mafunzo ya muda mfupi na ushauri katika teknolojia za uvuvi na ukuzaji viumbe kwenye maji. Kampasi hii inatekeleza majukumu muhimu katika kutoa elimu, mafunzo, na ushauri wa uvuvi na ukuzaji viumbe maji katika mikoa ya Kusini kando ya Bahari ya Hindi.
Kozi Zinazotolewa katika Kampasi ya Mikindani
Kozi Ndefu (Muda wa Miaka 3)
Kwa sasa, kampasi bado haijaanza kutoa mafunzo ya kozi ndefu kutokana na kutokidhi vigezo vya NACTVET.
Kozi Fupi (Kozi Maalum)
-
Mbinu bora za ufugaji wa majongoo bahari
-
Mbinu bora za kilimo cha mwani
-
Mbinu bora za kunenepesha kaa
-
Mbinu bora za ufugaji wa kambale
-
Mbinu bora za ufugaji wa kambale
-
Mbinu bora za ufugaji wa kamba koche
-
Mbinu bora za ufugaji wa sato kwenye maji ya chumvi
-
Uongezaji thamani wa mazao ya uvuvi ikiwemo mwani na samaki wenye thamani ndogo sokoni
-
Mbinu bora za kuzalisha nzi-chuma na ujenzi wa miundombinu yao
-
Mbinu bora za uzalishaji wa lulu
Mahali
Mikindani Campus is located in Mirumba street, Jangwani ward, along the coast of the Indian Ocean in the Mtwara region.
-
Mratibu wa Kozi: Salma Mwishaha Chatto, 0677559382, salma.chatto@feta.ac.tz
-
Meneja wa Kampasi: Issack Herman Tarimo, 0655827466, issack.tarimo@feta.ac.tz
-
S.L.P 62, Mtwara Mikindani
-
Barua Pepe: mikindani@feta.ac.tz
