KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI BI AGNESS MEENA AMEITAKA FETA KUENDANA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI NA KITEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA MAFUNZO.
Bi Meena ametoa kauli hiyo 25 Novemba, 2026 Posta jijini Dar es salaam wakati akifungua kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji kupitia na kujadili rasimu ya mitaala 5 iliyohuishwa na 12 inayopendekezwa kuanzishwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) .
"Mabadiliko ya Uchumi na Teknolojia yanatutaka kubadilika pia kwa namna tunavyoandaa vijana wetu" Amesema Bi Meena
Aidha amewataka wadau walioshiriki kupitia mitaala hiyo kuzingatia mambo Muhimu wakiwa wanapitia mitaala hiyo.
Akiyataja mambo hayo amesema Mafunzo yatakayotolewa yalenge katika utoaji wa mafunzo kwa vitendo, Mafunzo yaendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Mafunzo yashirikishe matumizi ya teknolojia za kisasa na zana mpya za uvuvi pamoja na Kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Pia amebainisha kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaendelea kutoa ushirikiano na kuweka mazingira wezeshi kwa FETA na wadau wengine katika kuimarisha shughuli za utoaji wa mafunzo ili yaweze kukidhi viwango na ubora uliokusudiwa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt. Semvua Mzighani amesema kuwa zoezi la wadau kupitia na kujadili mitaala hiyo linafanyika ikiwa ni mchakato wa kabla ya mitala hiyo kupelekwa NACTVET kwaajili ya utekelezaji.
amesema kuwa Uhuishaji wa mitaala 5 na mapendekezo ya kuanzisha mitaala mipya 12 yametokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, Ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa pia ni takwa la NACTVET Kuhuisha mitaala kila baada ya miaka 5.
Wadau waliokutana kupitia Mitaala Inayohuishwa na inayopendekezwa kuanzishwa na FETA ni kutoka taasisi za SUA, UDSM,NEMC,NIT, MLF,TANLAPIA,TAFIRI,OFISI YA RAIS UTUMISHI, SEKRETARIETI YA AJIRA, TASFAM, TASAC,TAFICO,LITA,